By Denis Kessy
Elisany Silva ni msichana mrefu kuliko wote duniani. Elisany silva alizaliwa tarehe 27 mwezi wa tisa mwaka 1995 katika jiji la Belem Brazil. Elisany ana urefu wa Futi sita na inchi tisa(6.9) sawa na sentimeta 206, urefu ambao unamfanya kuwa kati ya wasichana warefu duniani akiwa na umri wa miaka 14 tu.
“ Nilianza kuongezeka urefu nilipokuwa na miaka 11 na mpaka sasa bado naongezeka siku hadi siku” alisema Elisany. “Urefu huu unaninyima raha kwa kweli, kwa sababu nashindwa kucheza na wenzangu, pia shule nimeshindwa kwenda na hata kuingia kwenye mlango wa nyumba yetu imekuwa tabu” ameongeza elisany.Urefu wa Elisany umemfanya akose haki yake ya msingi kama mtoto, kwenda shule kusoma na kumfanya abaki nyumbani akisoma mwenyewe, kwa kile kinachosemwa kuwa, hakuweza kuingia kwenye basi la shule kutokana na urefu wake huo.
Madaktari wanasema elisany anaugua ugonjwa wa “Giantism” ugonjwa ambao unafanya viungo vya mwili kukua isivyo kawaida. Wanaamini kwamba kukua huko kunasababishwa na kutofanya kazi kwa baadhi ya hormoni na glandi za pituitari. Mara kwa mara Elisany amekuwa akilalamika maumivu ya kichwa na baadhi ya sehemu za miguu yake. Madaktari wanasema kwamba kama kukua huko hakutazuiwa, ataendelea kukua na kuhatarisha maisha yake..
“Nataka aache kukua ili awe sawa na wasichana wenzake,maana mara nyingine anajiskia vibaya kwa kuwa jinsi alivyo” alisema mama yake mzazi aitwaye Anna Maria Cruz. Wazazi wa Elisany ni maskini na hawana uwezo wa kugharamia matibau ya Elisany, Hali inayozidi kumchanganya Elisany alinye na ndoto kubwa ya kuwa mwanamitindo maarufu.
Suala la urefu wa Elisany limeanza kumfaidisha kwani baadhi ya makamouni ya mitindo yameanza kuonyesha dhamira ya wazi ya kumtumia mrembo huyo katika matamasha yao ya mitindo katika siku za karibuni. Endapo Elisany atafanikiwa katika ndoto yake hiyo ya mitindo, ataweza kijigharamia matibabu yake ambayo ya gharimu kiasi kikubwa cha pesa.
Taarifa zinasema kwamba elisany silva atashiriki kwa mara ya kwanza katika tamasha la mitindo katika jiji la Belem Nchini Brazil mwezi ujao.
elisany silva akiwa katika pozi
Elisany akiwa na rafiki zake ufukweni


No comments:
Post a Comment